We learn and Gain more knowledge on academic staffs

Monday, August 19, 2024

KAULI YA EDO KUMWEMBE KUHUSU AISHI MANULA

 


"Aishi kukaa nje hakulisaidii taifa. kuna mchuano mkubwa katika nafasi za ndani lakini sio katika nafasi ya langoni. Aishi anahitaji kucheza soka. Anahitaji kuwa langoni. Anahitaji kucheza. Hili sio jambo la masilahi yake binafsi bali ni kwa masilahi ya taifa.
.
“Wakati mwingine taifa linapaswa kuingilia kati mambo kama haya kwa masilahi ya taifa. kuna wakati Wabrazil walimwambia Neymar lazima aende akacheze soka la kulipwa Ulaya ili awe na uzoefu wa kutosha kuelekea kombe la dunia la mwaka 2014 ambalo lingefanyika nchini kwao Brazil mwaka 2014.
.
“Ndiyo maana Neymar aliondoka Brazil kwenda kucheza Barcelona mwaka 2013. Hii ni kama ilivyo kwa Aishi kwa sasa. Tunakabiliwa na michuano ya kufuzu kwenda Afcon mwaka 2025. Tunakabiliwa na michuano ya Afcon 2027 ambayo sisi tutakuwa wenyeji. Aishi anapaswa kuwa langoni.” — Edo Kumwembe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages

SoraTemplates

Best Free and Premium Blogger Templates Provider.

Buy This Template