KWA MJIBU WA @dicksonmpilipili
PINI 10 YA MAMBO NILIOYAONA SIMBA DHIDI YA TABORA UNITED

Ilikuwa ni mechi nzuri kuitazama licha ya changamoto za Tabora United lakini wameonyesha ushindani waliwapa heshima Simba wao wakisubiri kujibu maswali kutoka kwa Simba

Kocha wa Simba bado hajajipata timu imeshindqa lakini inakosa ubunifu na combination play katika safu ya ushambuliaji,anaonekana ni kocha anayeamini katika kushambulia kwa tahadhari

Abudlazak Hamsa ni mbadala sahihi amemzidi kwa kiwango Kennedy Juma dude ni beki wa kisasa anakaba na kushambulia yupo tough sana combination yake na Che Malone imekubali,washambuliaji wa Tabora United walipata wakati mgumu

Kama sio ubora wa Harun Mandanda na kukosa utulivu kwao leo hii Simba walikuwa wanapata mabao mengi ,Mandanda leo alikuwa katika ubora wake

Jean Charles Ohuoa ni mchezaji mzuri lakini sio smart na anakosa uwezo wa kusoma mazingira ya mchezo,Kuna mida alitakiwa kurahisisha mchezo ahawa anafanya maamuzi ya pupa,nw kuna muda akihitaji kutoa pasi kwa haraka anakaa nayo yeye aliikosesha Simba mabao mengi (Ana mkaba Mukwala)

Kuingia kwa Awesu Awesu leo ilikuwq ni msaada kwa Simba walipata umiliki wa mchezo sasa tunaelewa kwanini Fadlu anamuelewa ni yeye liyewaunganisha Simba eneo la kiungo na ushambuliaji achana na lile bao alilofunga anza kuangalia ile firt touch aliyoifanya ndani ya 18

bao la namna hii amewahi kuwafungq Yanga akiwa Kagera Awesu ni Fundi


Simba wametibu changamoto ya eneo lao la kiungo Debora Fernandez yupp tough na smart sana kama naona Okejepha achanganya wanaweza kuunda Combination nzuri,Mhesa,Seseme na wenzae wamepata wakati mgumu wa kutimiza majukumu yao katika mid-block

Valentino Mashaka bado ataendelea kuwa kuni ya akiba mbali na bao alilofunga dakika 30 alizocheza hakuwa hatari na hakuweza kuonyesha mikimbio wala uwezo binafsi anasafari ye kujitafuta

Endwin Balua no doubt huyu ni anakuja kuchukua namba ya kudumu anakupa ubunifu ,kasi na utulivu alikuwa ni kipimo sahihi cha umri wa Salum Chuku

Kibu Denis anajambo moyoni nq kitu mguuni,kuchelewa kuuungana na timu kumemuathiri anaonyesha kumuelewa Fadlu anataka nini,usimkatie mtu tamaa Kibu bado nyie
No comments:
Post a Comment